NYORO: SIJUI KWANINI NILIFURUSHWA

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amesema hajui sababu ya kutimuliwa kwake kutoka wadhifa wa mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa, akisisitiza kuwa hajawahi kuzungumziwa na mtu yeyote kutoka mrengo wa Kenya Kwanza kuhusu wadhifa huo.
Akizungumza na wanahabari afisini mwake katika majengo ya bunge, Nyoro vile vile amedinda kuzungumzia uhusiano wake na viongozi wengine wa kisiasa, akiwataka viongozi kuangazia utendakazi kwa wananchi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa