#Local News

MWANAMKE, 37, AHUKUMIWA MIAKA 25 ELDORET

Mahakama kuu mjini Eldoret imempa kifungo cha miaka 25 gerezani, mwanamke kwa jina Winnie Wangare Maina mwenye umri wa miaka 37 ambaye amepatikana na hatia ya kumwua mmewe kwa kumdunga kisu.

Akitoa hukumu hiyo, jaji Reuben Nyakundi amesema Ushahidi uliotolewa umethibitisha kwamba mshtakiwa alimwua Wycliffe Miriti mnamo mwezi oktoba mwaka 2022 walipokuwa ndani ya nyumba yao.

Jaji huyo aidha ametupilia mbali ombi la wakili wa mshtakiwa akitaka apewe kifungo cha nje.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *