TUPO TAYARI

Katibu Mkuu katika wizara ya Michezo Peter Tum amethibitisha kuwa serikali itaunga mkono tu mashirikisho yanayozingatia sheria zinazoongoza utendakazi wao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Nairobi City Marathon hapo jana, TUM alisisitiza umuhimu wa uwazi na uwajibikaji katika mashirikisho ya michezo.
Tum pia alisisitiza kuwa mashirikisho lazima yapeane kipaumbele maendeleo ya chipukizi katika taaluma zote.
Maoni ya Tum yanajiri huku kukiwa na wito wa kuangaliwa upya kwa Sheria ya Michezo ya 2013, ambayo baadhi ya vilabu na mashirikisho yanasema ni vigumu kuizingatia kikamilifu.
Imetayarishwa na Nelson Andati