CHELUGUI AZUNGUMZIA UPORAJI WA HUSTLER FUND

Waziri wa vyama vya ushirika na biashara ndogo ndogo Simon Chelugui amepuzilia mbali ripoti za matumizi mabaya ya fedha za mikopo ya hazina ya Hustler.
Katika kikao na wanahabari, Chelugui amesema kwamba madai yaliyoibuliwa na Wakenya kuhusu utoaji mikopo kwa njia isiyofaa na kusababisha kufujwa kwa mamilioni ya fedha ni ya uongo.
Kulingana na Chelugui, hakuna hata shilingi moja iliyofujwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa