UJERUMANI YAKABWA KOO

Mchezaji Niclas Fullkrug aliyetokea benchi aliifungia Ujerumani bao la kusawazisha dakika za lala salama walipookoa sare ya bila kufungana na Uswizi hadi kileleni mwa Kundi A.
Uswizi walikua na matumaini ya kuingia hatua ya 16 bora wakiwa washindi wa kundi baada ya bao la mapema kutoka kwa Dan Ndoye ila Fullkrug akawatoa matumaini hayo
Lilikuwa pigo kwa Uswizi, ambao walikuwa wamejilinda kwa uthabiti kwa zaidi ya dakika 90 lakini bado wanaendelea na hatua ya mtoano.
Ndoye pia alifungiwa bao la kuotea katika kipindi cha pili ambalo lingefanya matokeo kuwa 2-0 – bao la pili kupigwa nje baada ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR) kuingilia kati kwa Mjerumani Robert Andrich.
Kwa kushinda Kundi A, Ujerumani itamenyana na timu itakayomaliza katika nafasi ya pili katika kundi la Uingereza Jumamosi ijayo.
Imetayarishwa na Nelson Andati