#Sports

NYOTA WA LIVERPOOL JOTA AUAWA KATIKA AJALI YA GARI!

Mshambulizi wa Liverpool, Diogo Jota amefariki dunia kufuatia ajali ya gari nchini Uhispania akiwa na umri wa miaka 28.

Jota aliripotiwa kuwa alikuwa akisafiri kwa gari na kaka yake Andre, ambaye pia ni mwanasoka mwenye umri wa miaka 26, wakati gari hilo lilipotoka nje ya barabara.

Tukio hilo lilitokea kwenye A-52 katika jimbo la Zamora, kulingana na ripoti nyingi za vyombo vya habari vya Kiingereza na Kireno.

Habari hiyo ya kusikitisha inakuja wiki mbili tu baada ya Jota kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Rute Cardoso huko Porto.

Jota alisajiliwa na Liverpool Septemba 2020 kutoka Wolverhampton Wanderers kwa ada ya zaidi ya pauni milioni 40.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *