WAKAZI KITALE WAHANGAIKA, WAKOSOA KeNHA
Wakazi wa Matisi kaunti ya Tans Nzoia waliotoa ardhi yao kuruhusu ujenzi wa barabara ya Kitale kuelekea Suam mpakani mwa Kenya na Uganda miaka miwili iliyopita, wamelalamikia fidia walioahidiwa na serikali.
Wakazi hao ambao maduka yao yalibomolewa kupisha ujenzi huo, wameitaka mamlaka ya barabara kuu nchini KeNHA kufanikisha malipo yao kulingana na mkataba wao na serikali.
Aidha, wamelalamikia kupitia mahangaiko kutokana na kucheleweshwa kwa fidia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































