RANGERS NJE

Rangers walitolewa nje ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya Dynamo Kyiv kufunga mabao mawili ndani ya dakika mbili za mwisho kwenye Uwanja wa Hampden Park kufuatia kupigwa kadi nyekundu kwa winga wa Rangers kijana Jefte.
Mabao ya Oleksandr Pikhalyonok na mchezaji mwingine wa akiba Nazar Voloshyn yanamaanisha Rangers wanashuka hadi kwenye Ligi ya Europa isiyo na faida kubwa kwa msimu wa pili mfululizo.
Wageni hao wa Ukraine wanatinga hatua ya muondoano ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili katika misimu mitatu na watamenyana na Salzburg baada ya washindi hao wa pili wa Bundesliga ya Austria kuishinda FC Twente kwa jumla ya mabao 5-4 kufuatia sare ya 3-3 mjini Enschede jana usiku.
Imetayarishwa na Nelson Andati