WAKAAZI WA MIGORI WALALAMIKIA KUMWAGIKA KWA KEMIKALI ZENYE SUMU KUTOKA KWA MIMEA INAYOSAFISHA DHAHABU

Wakaazi wa eneo la Oruba-Siany kaunti ya Migori wameibua wasi wasi wao kufuatia kumwagika kwa kemikali zenye sumu kutoka kwa baadhi ya mitambo ya uchenjuaji dhahabu katika eneo hilo.
Wakaazi hao sasa wanatafuta uingiliaji kati wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA) huku wakisema wanyama wao wamekufa baada ya kunywa maji yaliyochafuliwa na zebaki kutoka kwa baadhi ya mitambo ya uchenjuaji katika eneo hilo.
Kwa mujibu wao kemikali zenye sumu kutoka kwenye mitambo ya uchenjuaji pia ni tishio kwa wananchi wanaoishi mkoani humo, na mazao yao
Imetayarishwa na Janice Marete