POLISI WA KENYA KUTUMWA HAITI NDANI YA WIKI – ASEMA RUTO

Mpango wa kuwatuma maafisa wa polisi nchini Haiti ungalipo licha ya kupingwa vikali na baadhi ya viongozi na mashirika ya kutetea hali za kibinadamu.
Haya ni kwa mujibu wa rais William Ruto akiongeza kuwa kenya ina uwezo wa kurejesha amani katika taifa la Haiti na kwamba maafisa hao watatumwa Haiti kulingana na mkataba wa makubaliano na baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Imetayarishwa na Janice Marete