KVA YAISUTA SERIKALI YA NAKURU

Chama cha madaktari wa mifugo nchini KVA kimekosoa mipango ya serikali ya kaunti ya Nakuru kufunga kichinjio cha mamilioni ya fedha cha Naivasha ili kupisha ujenzi wa makazi ya bei nafuu na uwanja wa michezo.
Kupitia taarifa, mwenyekiti wa chama hicho Kelvin Osore ameitaja hatua hiyo kuwa dharau kwa juhudi za serikali kuimarisha viwanda nchini, akisema kichinjo hicho hutegemewa kiuchumi na wafanyakazi 2,000 wanaolisha familia 10,000.
Aidha, Osore amesema kufungwa kwa kichinjo hicho kutaathiri wafanyakazi na wenyeji kwa jumla.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa