#Local News

AKAUNTI YA UDA YA FACEBOOK YADUKULIWA, MALALA

Katibu  Mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala ameibua madai kwamba ukurasa wa Facebook wa Chama hicho umedukuliwa na watu wasiokuwa wanachama wa baraza la uongozi na kwamba tayari amewasiliana na makao makuu ya mtandao huo ili kurekebisha hali

Hata hivyo mtaalamu wa mtandao wa rais William Ruto Dennis Itumbi amepuuza kauli ya Malala akisema kwamba mitandao yote ya UDA ipo shwari na kwamba hakuna cha kuhofia

Kauli hizo kinzani zinazidi kuibua mkanganyiko hata zaidi katika usimamizi wa chama hicho cha UDA hasa katika swala la ni nani anayepaswa kuzungumza kwa niaba ya chama hicho

Taarifa ya Malala inajiri baada ya kukosa kuelewana na bodi ya kitaifa ya uchaguzi ya UDA kuhusu uchaguzi wa mashinani katika kaunti ya Pokot Magharibi , Malala akitangaza kuwa uchaguzi huo umeahirishwa

Mwenyekiti ya bodi ya kitaifa ya uchaguzi wa UDA antony Mwaura alipuuzilia mbali kauli ya Malala akisema hana mamlaka ya kutoa tangazo hiyo

Kauli ya Mwaura iliwekwa katika mtandao wa FB ambao umezidi kuibua mkanganyiko mwingine baada ya ule wa juzi uliowahusisha baadhi ya viongozi akiwemo gavana wa kaunti ya Nyeri Mutahi Kaiga kuon ywa dhidi ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.\

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *