#uncategorized

VITAMBULISHO VYA WAKENYA KUHARIBIKA BAADA YA MIAKA 10

Wakenya watahitajika kubadilisha vitambulisho vyao kila baada ya miaka 10, katibu katika idara ya uhamiaji Julius Bitok akisema ilivyo kwa kadi za ATM, kijipande cha silikoni ambacho kinawekwa ndani ya vitambulisho hivyo mpya huharibika baada ya muda huo wa miaka 10.

Katika taarifa kwa wanahabari, Bitok ametetea hatua ya serikali kuleta vitambulisho vya kidijitali, akisema mataifa kama vile Uganda, Tanzania, Senegal na Ufaransa tayari yamekumbatia vitambulisho hivyo.

Aidha, amesema zoezi la uchapisho wa vitambulisho limeimarika baada ya idara hiyo kupokea printa mpya yenye uwezo wa kuchapisha stakabadhi hizo 30,000 kila siku.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

VITAMBULISHO VYA WAKENYA KUHARIBIKA BAADA YA MIAKA 10

WALUKE AWAONYA WAKAZI DHIDI YA KUANDAMANA

VITAMBULISHO VYA WAKENYA KUHARIBIKA BAADA YA MIAKA 10

POLISI WANASA PIKIPIKI 59 ZILIZOIBWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *