WAKAZI WAMWUA MSHUKIWA KOROKORONI

Wakazi waliokuwa na ghadhabu wamevamia kituo cha polisi cha Gachocho kaunti ya Murang’a na kumwua mshukiwa anayetuhumiwa kumwua ndugu yake.
Kulingana na ripoti ya polisi, wakazi hao wamevamia kituo hicho mchana huu baada yao kubaini kwamba mshukiwa huyo amekuwa akizuiliwa kwenye kituo hicho.
Baada ya makabiliano baina ya polisi na wakazi, wamefanikiwa kuingia ndani ya seli na kumchukua mshukiwa huyo kabla ya kumwua huku wakiharibu gari la polisi kwa mawe.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa