NATEMBEYA; TUSIJIUE TUKIKUMBWA NA MFATHAIKO

Shughuli ya kutafuta mwili wa mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyezama katika mto wa Koitobos ingali inaendelea.
Kwa mujibu wa barua aliyoandika Mwanafunzi huyo inadaiwa kuwa alijirusha katika mto huo kutokana ka msongo wa mawazo.
Gavana wa kaunti hiyo George Natembeya amefika eneo la Tukio ambapo ameahidi kuwatuma wapiga mbizi zaidi kusaidia katika shughuli hiyo.
Natembeya aidha amewarai wakaazi kutafuta ushauri nasaha wanapokumbwa na mfathaiko badala ya kujitoa uhai.
Imetayarishwa na Janice Marete