KNUT YAMTAKA RAIS RUTO KUSHUGHULIKIA GEN-Z
Chama cha Kitaifa cha Walimu (KNUT), tawi la Kisumu, kimeitaka serikali kuharakisha kushughulikia madai ya Gen- Z kukomesha maandamano na kurejesha hali ya kawaida huku shule zikifunguliwa baada ya likizo fupi.
Akihutubia wanahabari, David Obuon, Katibu Mtendaji wa KNUT tawi la Kisumu, amesema kuwa shule nyingi za mijini zinategemea usafiri wa umma, na kutokana na maandamano yanayoendelea, wanafunzi wengi wamekwama huku wengine wakilazimika kusalia nyumbani.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































