GORMAHIA WAONDOLEWA KWA MICHUANO YA CECAFA

Mabingwa wa ligi kuu nchini Gormahia jana jumanne waliondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa ya CECAFA inayoendelea baada ya kucharazwa 2-0 na Al -ILHAL ya Sudan.
Kogalo tayari walikuwa katika hati hati ya kuondolewa baada ya kukosa kupata ushindi katika mechi mbili.
Baada ya kipindi cha kwanza bila bao Al Ilhal walipata afueni katika kipindi cha pili kupitia kwa Mohamed Abdrahman ambaye alisababisha bao la kwanza na ahmed alhasan akifunga la pili.
Gor sasa wataelekeza jitihada zao katika ligi ya mabigwa wa CAF na vile vile msimu mpya wa ligi humu nchini.
Imetayarishwa na Janice Marete