#Local News

LORI LA KUBEBA GESI LALIPUKA PIPELINE, EMBAKASI

Wakazi mtaani Pipeline jijini Nairobi wameingiwa na hofu baada ya lori la kusafirisha gesi ya kupikia kulipuka karibu na kituo cha magari cha Stage Mpya.

Tukio hilo limewalazimu watoaji wa huduma za dharura kufika eneo hilo kuwahamishia maeneo salama waathiriwa waliokuwa wamefunikwa na moshi mkubwa

Kamanda wa polisi Adamson Bungei amesema bado wanachunguza chanzo cha mlipuko huo, ambao umejiri miezi kadhaa baada ya mlipuko mwingine kutokea katika eneo la Embakasi

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *