CAF YAKIRI UGUMU WA KUPANGA RATIBA YA MICHEZO
Waandalizi wa mashindano ya kandanda ya kimataifa ya wanaume na wanawake wamekiri kuwa wanakabiliwa na kibarua kigumu kupanga ratiba, lakini tarehe za matoleo yajayo zinakaribia kuafikiwa.
Veron Mosengo-Omba, ambaye ni katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), aliahidi kwamba tangazo kuhusu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (Wafcon) 2024 nchini Morocco lingetolewa mwishoni mwa mwezi huu – akifichua kuwa kuna uwezekano mkubwa inaweza kubadilishwa hadi mwaka ujao.
Wakati huo huo, Mosengo-Omba alithibitisha kwamba Caf inaweza kuandaa Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025, ambazo pia zitaandaliwa na Morocco, mapema 2026 kwa sababu ya muda wa Fifa wa Kombe la Dunia la Vilabu lenye timu 32 mwezi Juni na Julai mwaka ujao.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































