#Local News

MASHARTI MAPYA KWA WALIMU WATARAJIWA

Tume ya kuwaajiri walimu TSC imetoa mapendekezo mapya kwa wanaolenga kusomea kozi za ualimu katika vyuo vikuu na taasisi za mafunzo ya ualimu, ikipendekeza kwamba anayetaka kufundisha katika shule za sekondari ya juu na sekondari msingi ni sharti awe na alama ya B+ na zaidi katika masomo mawili anayotaka kufunza.

Kupitia taarifa, TSC imesema kwamba walimu watapata mafunzo kwenye masomo 3 yaliyo kwenye mtaala wa umilisi CBC, mwalimu anayetaka kufundisha sayansi akihitajika kusomea somo moja la sayansi ya kijamii.

Aidha, wanaolenga kufundisha sayansi katika sekondari msingi watahitajika kuwa na alama za C na Zaidi katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza, Hesabu na Kemia, kozi ya digrii ikichukua miaka 5 unusu na wala si miaka 4 jinsi ilivyo sasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MASHARTI MAPYA KWA WALIMU WATARAJIWA

EACC YAPATA MKUU MPYA

MASHARTI MAPYA KWA WALIMU WATARAJIWA

TUMEMSAMEHE MUUAJI, FAMILIA YA IAN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *