#Sports

MBOYA AJIVUNIA KUSHINDA TAJI

Faith Mboya, mshambulizi wa klabu ya Kibera Soccer Women, anajivunia kushinda taji la kombe la shirikisho la FKF na pia kumaliza katika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi kuu ya kina dada, katika msimu wake wa kwanza na timu hiyo.

Mboya hana shaka kwamba angeibuka mfungaji bora iwapo angeshiriki ligi hiyo kuanzia mwanzo.

Vile vile, mchezaji huyo anafurahia kuwakilisha timu ya taifa, Harambee Starlets, kwa mara ya kwanza, huku akifichua kuwa kwa sasa analengwa na klabu kadhaa za humu nchini na kutoka Tanzania.

Faith Mboya alijiunga na Kibera Soccer Women katika mkondo wa pili wa msimu akitokea Sunderland Samba ya NSL, ambapo mchango wake mkubwa uliisaidia timu hiyo kutwaa kombe la shirikisho la FKF.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MBOYA AJIVUNIA KUSHINDA TAJI

MURUNGA AKASHIFU MIZOZO YA RAGA

MBOYA AJIVUNIA KUSHINDA TAJI

KENYA KUANDAA PARA VOLLEY

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *