MALKIA WAANZA NA MIKOSI
Malkia Strikers walianza vibaya Michezo ya Olimpiki ya Paris Jumatatu alasiri, kwa kufungwa seti 3-0 na mabingwa mara mbili Brazil katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi B Uwanja wa Kusini mwa Paris Arena 1 nchini Ufaransa.
Malkia Strikers, walipoteza kwa seti za moja kwa moja 25-14, 25-13, na 25-12 dhidi ya taifa hilo linalo orodheshwa la pili duniani na washindi wa medali ya fedha katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo.
Hiki kilikuwa kipigo cha nane ambacho Malkia ilionja mikononi mwa Brazil katika mikutano nane.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































