#Local News

CHANGAMOTO YA WENYE CHANGAMOTO KWA SERIKALI

Jamii ya watu walio na changamoto za kimaumbile katika kaunti ya Trans Nzoia wameshinikiza katiba kufanyiwa marekebisho na kubuni wadhifa maalumu ili mwakilishi wao apigiwe kura moja kwa moja kwenye uchaguzi mkuu.

Katika kikao na wanahabari baada ya kukamilika kwa warsha iliyoandaliwa na shirika moja eneo hilo, viongozi wa jamii hiyo akiwemo Tom Juma wamesema vyama vya kisiasa vimekuwa vikikiuka sheria za uteuzi na kuwateua watu wasio na changamoto za kimaumbile kuiwakilisha jamii hiyo katika mabunge ya kaunti.

Naye mwenyekiti wao Ojiambo Opisa ameitaka serikali ya kaunti hiyo kubuni sera ya kushughulikia maslahi yao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CHANGAMOTO YA WENYE CHANGAMOTO KWA SERIKALI

SHIF NI HARAMU

CHANGAMOTO YA WENYE CHANGAMOTO KWA SERIKALI

LSK YAIPONDA IPOA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *