#Local News

MOSES KURIA AWASUTA MAWAKILI HAVI, AHMEDNASIR

Aliyekuwa Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria ametoa karipio kali kwa aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria LSK Nelson Havi na wakili Ahmednasir Abdullahi kwa kutoa maoni kwamba mawaziri wote waliofutwa kazi hawafai kushikilia nyadhifa zozote za serikali baada ya kufutwa kazi na Rais William Ruto.

Akijibu gazeti la serikali kuhusu kutimuliwa kwa Mawaziri 21 wa Ruto, Havi aliandika kwenye X kwamba kufutwa kazi “kunamaanisha kuwa hawastahiki kushikilia wadhifa wowote wa umma milele: kuteuliwa au kuchaguliwa.”

Wakili huyo aliongeza kuwa Mawaziri waliofukuzwa, akitoa mfano wa sheria, wako katika kundi moja na Magavana waliotimuliwa au Majaji walioonekana hawafai kuhudumu.

Imetayarishwa na Janice Marete

MOSES KURIA AWASUTA MAWAKILI HAVI, AHMEDNASIR

MUDAVADI AWARAI WAKENYA KUSITISHA MAANDAMANO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *