WALIMU WA JSS WADAI KUPEWA KANDARASI YA KUDUMU NA TSC

Walimu wa sekondari ya msingi JSS wamefanya maandamano katika kaunti mbali mbali humu nchini kushinikiza serikali kuwaajiri kwa kandarasi ya kudumu.
Kulingana na walimu hao tume ya huduma za walimu TSC imekiuka agizo la mahakama kuitaka kuwapa kandarasi ya kudumu baada ya kuhudumu kama walimu wanagenzi kwa Zaidi ya mwaka mmoja unusu
Maandamano hayo yanajiri wakati ambapo shule zimefunguliwa leo hii kwa muhula wa pili hali ambayo inatishia kulemaza mtaala wa umilisi CBC.