HAKUNA MALIPO KWAKO
Waziri wa michezo Onesmus Kipchumba Murkomen amesema serikali haitaendelea kumlipa kocha mkuu wa Harambee Stars Engin Firat baada ya kushindwa kuisaidia timu ya taifa ya soka Harambee Stars kufuzu katika kipute cha mwaka ujao cha kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) na badala yake watampiga kalamu.
Murkomen akizungumza hapo jana kwenye makao makuu ya wizara hiyo katika jengo la Talanta Plaza, Nairobi wakati wa uzinduzi wa jopo kazi la kukagua na kurekebisha sheria ya michezo ya mwaka wa 2013 alieleza shinikizo anazopata kutoka kwa wakenya za kumpiga kalamu kocha huyo kwa kufeli kutimiza wajibu wake na kusema wakati sasa umefika kumtimua kwa kutumia sheria.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































