MAAFISA BANDIA WA EACC WAKAMATWA KWA KUWALAGHAI POLISI, KUWANYANYASA WAMILIKI WA MADUKA
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imewakamata watu wawili wanaoshukiwa kuwavamia na kuwaibia wamiliki wa maduka mjini Mombasa.
Kulingana na EACC, washukiwa hao wanaaminika kuwa sehemu ya harambee ya wanachama watano ambayo inafanya kazi chini ya shirika la kibinafsi.
Shirika hilo aidha linasemekana kuwalenga wamiliki wa biashara kwa kujifanya wakaguzi wa Kupambana na Bidhaa Bandia ili kuwaibia pesa.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































