#uncategorized

SERIKALI IMEWEKEZA PAKUBWA KATIKA KILIMO ILI KUTATUA UHABA WA CHAKULA NCHINI

Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Ndindi Nyoro amesema serikali imewekeza pakubwa katika sekta ya kilimo ili kufanikisha mpango wa utoshelezi wa chakula nchini.


Kwa mujibu wa Nyoro bunge linabuni sheria ya kudhibiti bidhaa zinazoagizwa nchini wakulima wakiwezeshwa kuzalisha baadhi ya bidhaa nchini ili kupunguza gharama ya uagizaji.

Aidha nyoro ambaye pia ni mbunge wa kiharu amedokeza kwamba serikali imeongeza mgao wa inua jamii kuwasaidia watu wenye umri wa miaka 70 na Zaidi na Watoto mayatima.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *