MAHAKAMA YATAKA USHAHIDI DHIDI YA NATEMBEYA
Wafanyikazi 3 wa serikali ya kaunti ya Trans nzoia wanadaiwa kukamatwa baada ya kuhudhuria mkao wa kesi ya ufisadi inayomkabili gavana wa kaunti hiyo George Natembeya.
Haya yamejiri huku mahakama ikiagiza upande wa mashtaka kwenye kesi hiyo kuwasilisha Ushahidi wanaolenga kutumia dhidi ya Natembeya baada yao kukosa kufuata agizo la kuwataka kufichua stakabadhi wanazolenga kutumia kwenye kesi hiyo.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Victor Awiti unadai kukabiliwa na changamoto kupata stakabadhi zinazohitajika kutoka kwa afisi za kaunti.
Imetayarishwa na Maureen Mukhobe
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































