#Boxing #Sports

UKOSEFU WA PESA KWA TIMU

Klabu ya Siaya inayoshiriki ligi kuu ya ndondi imekosa kusafiri kwa mkondo wa pili wa ligi kuu ya Shirikisho la Ndondi nchini, mkondo unaoandaliwa mjini Mombasa wikendi hii.

Kulingana na kocha mkuu wa Siaya Top Rank Boxing Club Bw Joseph Ochieng’, klabu hiyo ilishindwa kusafiri hadi katika jumba la kijamii la Changamwe Mombasa kutokana na changamoto za kifedha.

Alisema walihitaji angalau Ksh. 50,000 kwa ajili ya usafiri na malazi ya mabondia watano, kiasi ambacho hawakuweza kukusanya.

Mchezo wa mkondo wa pili wa Shirikisho la Ndondi la Ligi ya Kitaifa ya Kenya utachezwa hadi Jumamosi Agosti 17, 2024 na umevutia timu 17 kutoka kote nchini huku mabondia 101 wakiwemo wanaume 90 na wanawake 11 wakitarajiwa kushiriki katika vitengo mbalimbali.

Timu nyingine ambazo pia zilishindwa kusafiri hadi Mombasa kutokana na changamoto za kifedha ni pamoja na klabu za Homa Bay na Busia Boxing lakini Bw. Ochieng’ ana matumaini kwamba zitaweza kushiriki mkondo wa Tatu wa Ligi ya Taifa ya Ndondi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

UKOSEFU WA PESA KWA TIMU

MTUTAMBUE KAMA WACHEZAJI

UKOSEFU WA PESA KWA TIMU

HATO APATIKANA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *