TUMEMSAMEHE MUUAJI, FAMILIA YA IAN
Tumemsamehe yeyote aliyehusika katika mauaji ya mtoto wetu, na hatutashinikiza kujua aliyehusika.
Ndiyo kauli ya familia ya Ian Sing’oei ambaye mwili wake ulipatikana katika eneo la Mwiki jijini Nairobi Jumamosi iliyopita, familia hiyo ikizungumza wakati wa mazishi ya kijana huyo.
Babake Ian, John Korir ambaye ni kamishna wa kaunti ya Elgeyo Marakwet na mamake ambaye ni afisa mkuu katika idara ya jinsia kaunti ya Bomet, wamesema kwamba hawana haja ya kumfahamu aliyemwua mtoto wao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































