#Local News

MGONJWA MMOJA WA MPOX AFARIKI DUNIA

Mtu mmoja amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Mpox huku jumla ya wagonjwa 13 wakiripotiwa tangu kugundulika kwa ugonjwa huo hatari nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Afya dkt Patrick Amoth amesema kuwa mgonjwa huyo alikuwa akipambana na matatizo mengine ya kiafya mwilini mwake.

Kesi hizo ziligunduliwa kutoka kwa sampuli 236 ambazo zilijaribiwa katika maabara na kesi hizo zilithibitishwa katika kaunti 10.

Amoth amezungumza haya wakati Wizara ya afya ilikuwa ikipokea msaada wa tembe milioni 15.2 za dawa za Neglected Tropical Diseases (NTDs) zenye thamani ya $1.6 milioni (Ksh.213M) kutoka kwa Shirika la Afya Ulimwenguni

Waziri wa afya Deborah Barasa amepongeza hatua hiyo, akibainisha kuwa mchango huo utasaidia pakubwa kudhibiti kuenea kwa NTDs katika taifa.

Imetayarishwa na Janice Marete

MGONJWA MMOJA WA MPOX AFARIKI DUNIA

KESI YA KUZUIA SENETI KUJADILI HOJA YA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *