WATU WAWILI WAJERUHIWA KIRINYAGA BAADA YA JENGO KUANGUKA
Watu wawili wamejeruhiwa baada ya jengo la ghorofa 2 lililokuwa likiendelea kujengwa kuanguka katika mtaa wa Gorobani kaunti ya Kirinyaga.
Kwa mujibu wa polisi watu wengine saba waliokuwa ndani ya jengo hilo wamefanikiwa kukimbilia usalama wao.
Mwakilishi wa wadi ya tebere Peter Karinga anasema mmiliki wa jengo hilo alikiuka utaratibu uliowekwa na mamlaka ya ujenzi NCA hivyo kusababisha udhaifu wa jengo hilo.
Vile vile Karinga ameishtumu serikali ya kaunti ya kirinyaga hasa idara ya ujenzi na miundo msingi kufuatia mkasa huo akidai kwamba baadhi ya waadisi wamekuwa wakichukua hongo na kuidhinisha ujenzi katika maeneo yasiyofaa.
Waadhiriwa wamekimbizwa katika hosipitali ya kimbimbi kwa matibabu ya dharura.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































