KENYA YAZUNGUMZIA KUFURUSHWA KWA KARUA
Serikali imetangaza kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi na wakenya kwa jumla wanatoa kauli za uchochezi, ikisema matamshi ya baadhi ya viongozi yanafufua makovu ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi, msemaji wa serikali Isaac Mwaura amewakosoa viongozi hao ambao hakuwataja, akisisitiza serikali itafanya kila iwezalo kuwahakikishia wananchi utulivu.
Aidha, Mwaura ametetea hatua ya serikali ya Tanzania kumfurusha kinara wa chama cha PLP Martha Karua kutoka nchini humo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































