GEORGIA KUTOA MAKALI YAO DHIDI YA SPAIN
Willy Sagnol ameonya kwamba Georgia itapambana dhidi ya Uhispania baada ya timu yake kuweka historia kwa kutinga hatua ya 16 bora ya Euro 2024.
Georgia wanakabiliwa na mtanange mgumu dhidi ya Uhispania walio katika fomu, baada ya kuwalaza Ureno 2-0 mjini Gelsenkirchen na kufuzu kutoka Kundi F katika mechi yao ya kwanza kabisa katika michuano mikubwa ya kimataifa.
Sagnol aliongeza kuwa bado anatatizika kuamini kile ambacho wachezaji wake walikifabya kwa kuwashinda mabingwa wa 2016 Ureno na kutinga hatua ya muondoano.
Uhispania ni moja wapo ya timu zenye kupigiwa upato kunyakua taji hilo baada ya kushinda Kundi B na alama tisa kamili, huko Cologne mnamo Jumatatu.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































