AHUKUMIWA MIAKA 150 KWA KUWAUA WANAWE

Mahakama ya Bomet imempa kifungo cha miaka 150 gerezani mwanamme mmoja baada ya kumpata na hatia ya kuwaua wanawe 3 mnamo mwaka wa 2019 katika kijiji cha Lelaitich kaunti ya Bomet.
Akitoa hukumu hiyo, jaji Julius Ng’arng’ar ameyataja mauaji hayo kuwa ya kinyama na kusema kuwa hukumu hiyo itatumika kama funzo kwa walio na nia ya kutekeleza uhalifu saw ana huo.
Hata hivyo, amempa mshtakiwa Benard Kirui uhuru wa kukata rufaa ndani ya siku 14.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa