#Basketball #Sports

TULIKOSA KUDHIBITI MCHEZO ASEMA KOCHA GENGA

Timu ya mpira wa vikapu ya Chuo Kikuu cha Nairobi, UON Terror, kocha mkuu Eugene Genga
ametaja ukosefu wa uthabiti kuwa sababu kuu iliyowafanya kupoteza pambano lao la wikendi
dhidi ya Umoja.

Wanafunzi hao walipoteza 64-75 katika mechi ya Ligi Kuu ya Kitaifa ya Wanaume iliyochezwa
kwenye Uwanja wa Nyayo Gymnasium.Genga pia ametaja usumbufu ambao haukutarajiwa
ambao uliyumbisha utulivu wao mbele ya ule muhimu kwa kupoteza kwao.

Terror kwa sasa wana pointi 11 baada ya kucheza michezo tisa, wakishinda miwili na kupoteza saba huku Umoja wakiwa na pointi 13 baada ya kucheza michezo nane, kushinda mitano na kupoteza.

Mabingwa watetezi, Nairobi City Thunder wanaongoza ligi kwa alama 20 baada ya kucheza
michezo kumi, wakishinda yote na kufuatwa kwa karibu na Mamlaka ya Bandari ya Kenya (KPA)
ambao wamecheza michezo kumi, kushinda minane na kupoteza miwili wakiwa na alama 18.

Imetayarishwa na Nelson Andati

TULIKOSA KUDHIBITI MCHEZO ASEMA KOCHA GENGA

KOCHA WA NZOIA ATAJA MAKOSA YA KIKOSI

TULIKOSA KUDHIBITI MCHEZO ASEMA KOCHA GENGA

PSG YALAZA LIVERPOOL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *