#Local News

UKAME WA MCCARTHY WAIBUA HOFU

Mkufunzi wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars Benni McCarthy ataendelea kusubiri ushindi tangu achukue hatamu za uongozi wa kikosi hicho, baada ya timu hiyo kutoka sare ya kutofungana dhidi ya Chad kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa nchini Moroko Jumamosi iliyopita.

Stars ambao wanashikilia nafasi ya 111 kwenye jedwali la FIFA, walianza mechi hiyo wakipigiwa upato wa kuibuka washindi, ilasare tasa ikamaanisha kwamba raia huyo wa Afrika Kusini sasa ameiongoza timu hiyo kwa mechi 3 bila ushindi, mwanzo akiandikisha sare ya mabao 3 dhidi ya Gambia, kichapo cha 2:1 mikononi mwa Gabon kabla ya sare ya wikendi iliyopita.

Stars ambao wanajiandaa kwa ajili ya kipute cha CHAN baadaye mwaka huu, watarudiana na Chad hapo kesho kwenye mechi nyingine ya kirafiki.

Akizungumza na wanahabari baada ya mechi hiyo, McCarthy amelalamikia ukosefu wa makali kwenye safu yake ya ushambulizi, akiwataka wachezaji wake kuonyesha makali wanapokuwa kwenye lango la mpinzani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *