#Local News

MAHAKAMA ELDORET YAWASAMEHE MAAFISA WANNE WA KAUNTI

Mahakama ya uajiri na leba mjini Eldoret imemsamehe katibu katika serikali ya kuanti hiyo Edwin Bett na maafisa wengine watatu wakuu kwenye kaunti hiyo kutokana na kosa la wanne hao kukataa kutii agizo la mahakama, ambalo sasa wamekubali kulitii.

Jaji Maureen Onyango alipaswa kuwapa wanne hao hukumu ya kifungo gerezani au faini baada yao kukataa kuwaajiri kwa kandarasi ya kudumu wafanyakazi 30 kama ilivyokuwa imeagiza mahakama hiyo mnamo mwezi Juni mwaka jana.

Wanne hao ni Bett Pamoja na Waziri wa afya katika serikali ya kaunti hiyo Sammy Kotut, aliyekuwa afisa wa huduma za afya Paul Wangwe na mkuu wa bodi ya utumishi wa umma kwenye kaunti Francisac Bowen

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAHAKAMA ELDORET YAWASAMEHE MAAFISA WANNE WA KAUNTI

MAHAKAMA YASITISHA UCHAGUZI WA KJSA

MAHAKAMA ELDORET YAWASAMEHE MAAFISA WANNE WA KAUNTI

RAIS BIDEN KUITEUA KENYA KATIKA NATO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *