#Business

MFUMO MPYA WA KILIMO WAINUA WAKULIMA WADOGO AFRIKA MASHARIKI

Kenya imetajwa kuwa kielelezo barani Afrika katika kuwezesha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wa mashamba madogo madogo, kufuatia mafanikio ya majaribio ya mfumo wa kifedha uliotekelezwa kwa kushirikiana kati ya Hello Tractor, na Heifer International. Kupitia mfumo wa lipa kadri unavyotumia kwa matrekta, wakulima na wajasiriamali wamepata fursa ya kujiendeleza kwa kutumia mashine bila kuhitaji mtaji mkubwa wa kuzinunua moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Aceli Africa ya mwaka 2024, iliyochambua zaidi ya mikopo 32,000 yenye thamani ya dola bilioni 1.98 kutoka mwaka 2020 hadi 2023, Hello Tractor imepata matokeo bora kuliko wakopeshaji wa kawaida. Kupitia uwekezaji wa dola milioni 2.5 kutoka Heifer, asilimia 76 ya mikopo 88 iliyotolewa ilikuwa kati ya dola 50,000 hadi 200,000 — na cha kuvutia zaidi, wakopaji wote wa mara ya kwanza nchini Kenya walilipa mikopo yao kikamilifu.

Mpango huu umejumuisha pia mafunzo kwa vijana wa ndani kuwa mafundi wa huduma za baada ya mauzo, kuhakikisha matrekta yanaendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza imani ya wakopeshaji. Kutokana na mafanikio hayo nchini Kenya, mfano huu wa kifedha sasa umepanuliwa hadi Rwanda, Uganda, Tanzania na Zambia — ukiwa mfano halisi wa jinsi ubunifu, uwekezaji sahihi, na ushirikiano vinaweza kuleta mabadiliko makubwa katika kilimo cha Afrika.

IImetayarishwa na Mercy Asami

MFUMO MPYA WA KILIMO WAINUA WAKULIMA WADOGO AFRIKA MASHARIKI

KITHURE AWAONYA WAPINZANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *