NAIROBI KUGHARAMIA KIFUA KIKUU, USAID YAJIONDOA

Katika juhudi za kuhakikisha wagonjwa wa kifua kikuu katika kaunti ya Nairobi wanaendelea kupokea huduma za matibabu dhidi ya ugonjwa huo, serikali ya kaunti hiyo italazimika kutafuta njia mbadala za kufadhili matibabu hayo hasa baada ya kubainika kuwa imepoteza zaidi ya shilingi bilioni 1 kutokana na kukatizwa kwa ufadhili wa shirika la Marekani la USAID.
Afisa mkuu katika wizara ya afya kwenye serikali hiyo Tom Nyakaba, amesema kaunti hiyo inakabiliwa na mzigo mkubwa wa kutoa matibabu ya ugonjwa huo kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa.
Aidha, wizara ya afya imehimiza uchunguzi wa kina ili kukomesha maradahi ya kuambukiza kufikia mwaka 2030.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa