ALIYEKUWA MPENZI WA MWANARIADHA REBECCA CHEPTEGEI DICKSON NDIEMA AMEFARIKI
Aliyekuwa mpenzi wa mwanariadha Rebeca Cheptegei Dickson Ndiema ameaga dunia
Hospitali ilithibitisha kuwa Ndiema amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) alikokuwa amelazwa.
Ndiema amefariki siku chache baada ya Cheptegei kufariki katika hospitali hiyo hiyo.
Ndiema alimvamia Cheptegei nyumbani kwake ambapo alimmwagia petroli na kumchoma moto ambao pia ulimjeruhi.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































