SERIKALI YAAHIDI KUBORESHA AFYA

Huku wengi wa wakenya wakilalamikia changamoto katika bima ya afya ya Taifa Care, serikali imeanzisha mikakati ya kutatua changamoto hizo mbali na kuboresha sekta ya afya kwa ujumla.
Kwa mujibu wa naibu rais Kithure Kindiki, miongoni mwa changamoto zinazotishia ufanisi wa bima hiyo ni hatua ya wengi wa waliojisajili kukosa kulipa ada zao.
Ameyasema haya katika kongamano la washikadau wa afya jijini Nairobi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa