TUWASHAURI WATOTO

Baadhi ya viongozi wa kidini wanaitaka serikali kupitia wizara ya elimu kuwapa ushauri nasaha wanafunzi ambao jamaa zao walifariki au kujeruhiwa katika janga la mafuriko.
Mwenyekiti wa kanisa la Kenya Evangelical Alliance tawi la Nandi Teddy Kisivuli amesema ni vyema kwa wanafunzi na walimu kupewa ushauri nasaha ili kuepuka msongo wa mawazo hasa shule zinapofunguliwa Jumatatu wiki ijayo.