#Local News

SERIKALI YALILIA WAZAZI KUHUSU MAANDAMANO

Serikali imepoteza mapato ya shilingi bilioni 6 kutokana na maandamano ambayo yameikumba nchi kwa takribani mwezi mzima sasa, msemaji wa serikali Isaac Mwaura akiwataka wazazi kuchukua usukani katika kukomesha maandamano hayo.

Katika kikao na waandishi wa habari jijini Nairobi, Mwaura amehofia kwamba huenda uchumi ukadorora zaidi iwapo maandamano hayo yataendelea.

Aidha, Mwaura amevitaka vyombo vya habari kutoegemea upande wowote wakati wa kuripoti matukio ya maandamano, akisisitiza kwamba serikali inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *