WIZARA YA AFYA KAUNTI YA TRANSNZOIA YAWAHAMASISHA WAKAAZI KUHUSU UMUHIMU WA CHANJO YA POLIO
Wizara ya afya katika kaunti ya Transnzoia inaendelea kuwahamasisha washikadau mbali mbali na wathiriwa wa kupooza kabla ya awamu ya pili ya chanjo dhili ya marathi ya pollio kuanza tarehe 9-13 mwezi huu kufanyika katika kaunti 9 kote nchini.
Mshirikishi wa uhamasishaji katika maswala ya afya ya kaunti hiyo Leah Okumu amesema kuwa ni muhimu kuwapa Watoto chini ya miaka 10 chanjo ili kuwalinda dhidi ya marathi hayo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































