SIJAKUWA NA MSAIDIZI, RAIS RUTO
Nimekosa wa kunisaidia kuwaeleza wakenya kuhusu miradi ya serikali na hivyo kuwa changamoto kuu katika serikali yangu kwa kipindi cha miaka 2 iliyopita.
Ni usemi wake Rais William Ruto akizungumza wakati wa kuapishwa kwa naibu rais wa tatu wa Kenya Kithure Kindiki katika ukumbi wa mikutano KICC jijini Nairobi.
Kwa mujibu wa Rais, Kindiki ana uwezo wa kujaza pengo analosema limekuwapo kwa kipindi hicho.
Kwa upande wake, Kindiki ameahidi kuchapa kazi ili kuona taifa linasonga mbele kimaendeleo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































