UCHUKUZI JOGOO WATATIZWA

Shughuli za uchukuzi zimetatizika kwa muda katika barabara ya Jogoo jijini Nairobi kufuatia maandamano ya wafanyabiashara waliofunga barabara hiyo na kuwasha moto karibu na makutano ya Likoni Road kulalamikia madai ya kuwepo kwa mpango wa kubomoa vibanda vyao.
Kulingana na wafanyabiashara hao, hawajapewa eneo mbadala la kuendeleza shughuli zao wakati ambapo vibanda vipya vitakuwa vikijengwa.
polisi wamelazimika kuwatawanya kwa vitoza machozi, huku wahudumu wa magari wakilazimika kutumia barabara mbadala.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa