#Business

EPRA: BEI ZA MAFUTA KUBAKI SAWA KWA MIEZI MITATU MFULULIZO.

Halmashauri ya Kudhibiti Bei za Bidhaa za Petroli (EPRA) imetangaza kuwa bei za mafuta zitasalia bila mabadiliko kwa mwezi wa tatu mfululizo.

Kupitia taarifa rasmi, EPRA imesema kuwa imeendelea kutumia hazina ya ustahimilivu wa bei ili kuzuia ongezeko la gharama ya bidhaa hizo.

Hii ina maana kuwa kuanzia usiku wa kuamkia leo, bei ya petroli jijini Nairobi itasalia kuwa Shilingi 174.63 kwa lita, dizeli Shilingi 164.86, huku mafuta taa yakiendelea kuuzwa kwa Shilingi 148.99 kwa lita.

SGR YAREKODI ONGEZEKO LA MIZIGO NA MAPATO YA ABIRIA.

Shirika la Reli la Kenya (KRC) limeripoti ongezeko la asilimia 40 katika mahitaji ya huduma ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya Reli ya Kisasa (SGR) katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Kulingana na ripoti iliyotolewa jana, SGR imesafirisha jumla ya tani milioni 1.82 za mizigo kati ya Januari na Machi, ikilinganishwa na tani milioni 1.3 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Wakati huo huo, mapato yatokanayo na huduma ya usafiri wa abiria yameongezeka hadi shilingi bilioni 3.82, kutoka dola milioni 25 mwaka jana.

Imetayarishwa na Marete Janice

EPRA: BEI ZA MAFUTA KUBAKI SAWA KWA MIEZI MITATU MFULULIZO.

ULINGO WA SIASA WAPATA MGENI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *