AL HILAL YASAMBARATISHA MANCITY

Kocha wa Al Hilal Muitaliano Simone Inzaghi aliipongeza timu yake ya “ajabu” baada ya ushindi wa Jumatatu wa mabao 4-3 katika muda wa ziada dhidi ya wababe wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City kwenye Kombe la Dunia la Vilabu.
Inzaghi alikuwa ameiongoza timu hiyo kwa siku chache tu kabla ya mchezo wa ufunguzi ambapo timu yake ilitoka sare na Real Madrid na kusema sifa ya kucheza ni ya wachezaji.City ilishinda michezo yao yote mitatu ya hatua ya makundi na baada ya ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Juventus katika mchezo wao wa mwisho kabla ya hatua ya mtoano walionekana kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania taji hilo.
Kocha wa City, Pep Guardiola alitoa sifa kwa Al Hilal lakini ni wazi hakuwa ameona matokeo kama hayo. Mhispania huyo alisifu jinsi timu ya Inzaghi ilivyowaumiza kwenye mashambulizi ya kaunta.
Imetayarishwa na Nelson Andati